Hedhi inastahili kuwa suala la faragha lakini sio siri

Chanzo cha picha, The Pink Protest
Wanawake wa matabaka mbali mbali wamekua wakisimulia masuala ya hedhi katika mitandao ya kijamii.
Hii ni sehemu ya mkakati wa kuhamasisha umuhimu wa kuzungumzia wazi wazi masuala ya hedhi matandaoni kwa kutumia hashtag #FreePeriodStories, ambayo wanaharakati wanaamini itasaidia kukabiliana na unyanyapaa unaozunguka suala hilo.
Watu wanazungumzia nini na kwanini mjadala huu ni muhimu?
Kwa wengine ni hadithi za kuchekesha na za kuabisha.
Emma aliwasilisha ujumbe huu kwa Twitter:
"Tafakari wakati unapomuelekeza rafiki yako jinsi ya kutumia tampon au taulo ya hedhi kwa mara ya kwanza, ukiwa umesimama nje ya choo, anatoka njee akionekana kuwa na wasi wasi, unamuangalia tena na kugundua bwanawee... nilitumia maneno ya kuaibisha... ndio hali ilivyo #freeperiodstories."
Mkala hii imebeba madhui yaliyotoka kwenye mitandao ya kijamii. Tunaomba ruhusa yako kabla kitu chochote hakija pakiwa, sababu wanaweza wakawa wanatumia Cookies na tekinolojia nyingine. Unaweza ukasoma sera sera ya kutumia cookies katika mitandao ya kijamii kabla ya kukubali. Kutazama maudhui haya chagua accept and continue
Mwisho wa X ujumbe, 1
Kwa wengine, kama Natasha, inamaanisha kuangazia suala hili kwa wanaume:
"Siku moja niliangusha mkoba wangu kwa bahati mbaya tampons saba zikatapakaa kwenye sakafu. Mpenzi wangu alipoinama kunisadia kuokota vitu vyangu vilivyomwagika, nakumbuka nilishtuka na kusema kwa sauti 'SI ZANGU!' Hadidhi yako ni gani#freeperiodstories");