Diamond Platnumz mmoja wa watakaotumbuiza tuzo za MAMA
Majina ya watakaotumbuiza kwenye tuzo za mwaka huu za MTV mamas yametangazwa. Tuzo hizo zitafanyika nchini Uganda tarehe 20 mwezi wa Februari . Miongoni mwa watakaoutumbuiza ni pamoja na Wizkid kutoka Nigeria, Sheeba Kirungi wa Ugana na Diamond Platnumza maarufu kwa kibao hiki kutoka Tanzania. Kwenye ukurasa wake wa Instagram Diamond ameandika kuwa atahakikisha ametumbuiza kwa njia ya kihistori itakayofanya bara Lote la Afrika kuwa na fahari.