Fahamu mambo matano ya kipekee kuhusu Papa mpya, Leo XIV

s

Chanzo cha picha, Getty Images

Kuchaguliwa kwa Kardinali Robert Francis Prevost kuwa Papa Leo XIV kumeweka historia mpya ndani ya Kanisa Katoliki.

Akiwa Papa wa kwanza kutoka Marekani, yeye ni kiongozi anayetajwa kuwa na mwelekeo wa kuendeleza mageuzi ya hayati Papa Francis, huku akisisitiza huduma kwa maskini na makundi yaliyo pembezoni.

Papa Leo XIV mwenye umri wa miaka 69, anakuwa kiongozi wa 267 wa Kanisa hilo akichukua nafasi ya Papa Francis aliyefariki mwezi uliopita. Uchaguzi wake unahitimisha minongo'ono ya nani kuwa Papa iliyodumu kwa majuma

Hapa tunakuletea mambo matano ya kipekee kuhusu maisha na utume wa Papa huyu mpya

1. Jina la Kipapa: Leo XIV

s

Chanzo cha picha, Getty Images

Maelezo ya picha, Papa mpya Leo XIV kulia akisalimia na Papa Francis aliyefariki dunia mwezi uliopita. Aliheshimika na kuaminika na Papa Francis wakati wa uhai wake

Uamuzi wa kuchukua jina "Leo XIV" si wa kawaida. Papa wa mwisho kutumia jina hilo alikuwa Papa Leo XIII aliyeliongoza Kanisa kati ya 1878 hadi 1903. Alijulikana kwa msimamo wake thabiti kuhusu haki za wafanyakazi na mafundisho ya kijamii ya Kanisa Katoliki.

Skip Iliyosomwa zaidi and continue reading
Iliyosomwa zaidi