Kanisa Katoliki lina utajiri kiasi gani na unatoka wapi?

g

Chanzo cha picha, Getty Images

Maelezo ya picha, Fedha za Kanisa Katoliki zimekuwa siri kila wakati.

Kulingana na msemo, thamani ya urithi wa Kanisa Katoliki ni moja wapo ya mafumbo ya imani, siri ambayo taasisi hiyo imehifadhi kwa karne nyingi.

Kwasababu ya usiri huu, uvumi juu ya kiwango cha utajiri wa Holy See umeongezeka mwaka baada ya mwaka, na kuunda fumbo karibu na mada ambayo inapakana na ujinga na maoni kama vile "kwa nini Papa hauzi Vatican kumaliza njaa duniani");