Papa Francis asema starehe ya tendo la ndoa ni 'zawadi kutoka kwa Mungu'

Chanzo cha picha, Getty Images
Kiongozi wa kanisa katoliki Duniani Papa Francis amesema kwamba furaha ya tendo la ndoa ni "zawadi kutoka kwa Mungu" ambayo inapaswa "kuwa na nidhamu na uvumilivu."
Pia alionya dhidi ya ponografia, ambayo alisema inawafanya binadamu "kuridhika bila kuingia katika uhusiano" na inaweza kusababisha uraibu.
Papa alikuwa akizungumza mbele ya hadhara yake kuu mjini Vatican siku ya Jumatano.
Hotuba hiyo ambayo ni sehemu ya mfululizo wa mahubiri kuhusu tabia mbaya na wema, ililenga kile Papa alichokiita “pepo wa tamaa”.
Papa alisema kwamba tamaa "huharibu uhusiano kati ya watu" na kuongeza kuwa "habari za kila siku zinatosha kuandika ukweli huu".
"Je, ni mahusiano mangapi ambayo yalianza kwa njia bora na baadaye yamegeuka kuwa mahusiano yenye sumu");