Afghanstan: Taliban yafunga vyuo vikuu kwa wanawake

G

Chanzo cha picha, Getty Images

 Taliban imetangaza kufungwa kwa masomo ya vyuo vikuu kwa wanawake nchini Afghanstan kulingana na barua ya wizara ya elimu ya juu. 

Waziri anasema hatua hiyo inachukuliwa hadi taarifa nyingine itakapotolewa baadaye. 

Taarifa hiyo ya wizara ya elimu ya juu pia inawazuia wanawake kupata elimu rasmi, kwa sababu tayari walikuwa wamezuiwa kuhudhuria masomo ya sekondari 

Mwanafunzi mmoja mjini Kabul ameiambia BBC kwamba amekuwa akilia tangu aliposikia taarifa hiyo. 

Miezi mitatu iliyopita maelfu ya wasichana na wanawake walifanya mtihani wa kujiunga na Chuo Kikuu kote nchini   Afghanistan.

Lakini masharti yaliwekwa kote  kuhusu masomo ambayo wangeyapata, huku wakiwekewa masharti magumu kabisa ya kujiunga na vitivo vya sayansi ya mifugo, uhandisi, uchumi na kilimo pamoja na uandishi wa habari.   

Baada ya Taliban kuchukua mamlaka mwaka jana, vyuo vikuu vilianzisha ubaguzi wa kijinsia katika vyumba vya madarasa  na milango ya kuingia vyuoni.

Wanafunzi wanawake walikuwa wakifundishwa tu na maprofesa wanawake pekee au wakufunzi wa kiume wa umri wa juu.

Akijibu kuhusu marufuku ya sasa, mwanafunzi mmoja wa kike aliiambia BBC kwamba alifikiri Taliban walikuwa wanahofia wanawake na mamlaka yao. 

 "Wamekata daraja pekee ambalo lingeniunganisha na hali yangu ya baadaye ‘’, alisema.

"Ninaweza kusema vipi? Ninaamini kwamba ningeweza kusoma na kubadili hali yangu ijayo au kuleta mwangaza kwa maisha yangu lakini wameuharibu."

Sekta ya elimu ya Afghanistan iliathiriwa pakubwa baada ya Taliban kuchukua utawala na kumekuwa na wasomi wachache waliopata mafunzo baada ya kuondoka kwa vikosi vilivyoongozwa na Marekani mwaka jana.    

Mwanamke mwingine alizungumzia kuhusu  "kupitia magumu mengi sana" alipojaribu kuendelea na elimu yake baada ya Taliban kuchukua mamlaka ya nchi.

Aliiambia BBC: "Tulipigana na makaka zetu, na mababa zetu, na jamii na hata na serikali.  

"Tulipitia hali ngumu ili tuweze tu kuendelea na elimu yetu. 

Wakati ule walau nilikuwa mwenye furaha kwamba ningeweza kuhitimu Chuo kikuu na kuafikia ndoto zangu. Lakini, sasa ninawezaje kujishawishi mwenyewe");