Je, Putin "ameitunza" Urusi katika miaka yake 25 madarakani?

.

Chanzo cha picha, Getty Images

Maelezo ya picha, Boris Yeltsin (kushoto) alitangaza mnamo Desemba 31, 1999 kwamba atajiuzulu mara moja na kukabidhi madaraka ya urais kwa Vladimir Putin.
  • Author, Steve Rosenberg
  • Nafasi, Mhariri wa Habari wa BBC Russia
  • Akiripoti kutoka Moscow

Sitasahau mkesha wa mwaka mpya 1999.

Nilikuwa nikifanya kazi kama mtayarishaji wa matangazo katika afisi ya BBC mjini Moscow wakati ghafla habari muhimu zilipotokea: Rais wa Urusi Boris Yeltsin alikuwa amejiuzulu.

Uamuzi wake wa kujiuzulu ulishangaza kila mtu, ikiwa ni pamoja na waandishi wa vyombo vya habari vya Uingereza mjini Moscow. Habari hizo zilipotokea, hakukuwa na waandishi wowote wa habari katika ofisi ya BBC, kwa hivyo nililazimika kuandika na kutangaza habari hiyo muhimu mimi mwenyewe.

Katika taarifa hiyo ya habari, niliandika: "Boris Yeltsin alikuwa akisisitiza kuwa atamaliza muhula wake wa urais. Lakini leo aliwaambia raia wa Urusi kwamba amebadilisha nia yake."

Na huo ndio ulikuwa mwanzo wa taaluma yangu kama mwandishi wa habari.

Na pia ulikuwa mwanzo wa utawala wa Vladimir Putin kama rais wa Urusi.

Kwa mujibu wa katiba ya Urusi, Waziri Mkuu Putin alichukua wadhifa wa urais baada ya Yeltsin kujiuzulu. Alishinda uchaguzi miezi mitatu baadaye.

Agizo la Yeltsin kwa Putin alipokuwa akiondoka kwenye ofisi ya rais huko Kremlin lilikuwa: "Linda Urusi!"

Na huku vita vya Urusi dhidi ya Ukraine vikiadhimisha miaka mitatu, nakumbuka maneno hayo ya Yeltsin kila mara.

Hii ni kwa sababu uvamizi wa Putin nchini Ukraine umekuwa na matokeo mabaya.

Madhara haya kimsingi yameathiri Ukraine, ambayo imeshuhudia uharibifu mkubwa wa miundombinu na vifo vya watu katika miji yake. Takriban asilimia 20 ya eneo la Ukraine limetwaliwa na Urusi, na takribani raia milioni 10 wamelazimika kuhama makazi yao.

.

Chanzo cha picha, Getty Images

Maelezo ya picha, Putin (kulia) anajionyesha kama mtetezi mamlaka ya Urusi kama rais, akisema Boris Yeltsin hakufanikiwa katika suala hili.

Lakini Urusi pia imepata hasara kubwa:

Tangu uamuzi wa Vladimir Putin wa kuanzisha kile anachokiita "operesheni maalum ya kijeshi" nchini Ukraine, Urusi imepata hasara kubwa katika uwanja wa vita.

Miji mingi katika nchi hii inalengwa mara kwa mara na mashambulizi ya ndege zisizo na rubani.

Uchumi wa Urusi pia unakabiliwa na shinikizo kutokana na vikwazo vya kimataifa.

Ukandamizaji wa kisiasa ndani ya Urusi umeongezeka, na wanajeshi wa Ukraine wamechukua udhibiti wa sehemu ya mkoa wa Kursk wa Urusi.

Nimekuwa nikiripoti kuhusu Putin tangu aingie madarakani robo karne iliyopita.

Mnamo Desemba 31, 1999, ni nani angefikiria kwamba kiongozi huyo mpya wa Urusi bado angekuwa madarakani miongo miwili na nusu baadaye? Au kwamba Urusi itakuwa katika vita na Ukraine na kukabiliana na mataifa ya Magharibi leo hii?

Mara nyingi huwa najiuliza ikiwa Urusi ingechukua mkondo tofauti wa kihistoria ikiwa Yeltsin angemchagua mtu mwingine kumrithi. Bila shaka, hili ni swali la nadharia. Historia ina tafakari nyingi kuhusu 'iwapo' au 'labda' ya mambo mengi.

Lakini jambo moja ninaloweza kusema kwa uhakika ni kwamba: katika kipindi cha zaidi ya miaka ishirini na mitano, nimeona Putin akibadilika na kuwa mtu wa aina nyingi tofauti.

Na sio mimi peke yangu niliyeshuhudia hili.

Mnamo 2023, Katibu Mkuu wa zamani wa muungano wa kijeshi wa NATO George Robertson aliniambia kuwa, "Putin niliyekutana naye, ambaye tulifanya naye biashara nzuri na ambaye tulianzisha baraza la NATO-Urusi, alikuwa tofauti sana na mtu huyu wa sasa anayejipiga kifua."

"Mtu aliyesimama karibu nami Mei 2002 na kusema kwamba Ukraine ni nchi huru yenye serikali yake ya kitaifa ambayo inajiamulia kuhusu usalama wake sasa ndiye mtu anayesema kwamba [Ukraine] sio nchi."

Anaendelea kusema: "Nadhani Vladimir Putin ni mtu ambaye ana maoni makubwa sana kwa nchi yake. Umoja wa Kisovieti ulikuwa nchi ya pili yenye nguvu zaidi duniani, lakini Urusi ya leo haiwezi kudai kuwa katika nafasi hiyo. Nadhani hili linamkera."

Hii inaweza kuwa sababu moja ya mabadiliko tunayoyaona kwa Putin: azma kuu ya "kuifanya Urusi kuwa kubwa tena" (na kufidia hatua ya kushindwa kwa Moscow katika enzi ya Vita Baridi) ambayo imeweka Urusi kwenye njia ambayo haina budi kuzozana na mataifa Jirani, pamoja na yale ya Magharibi.

Lakini Kremlin ina maelezo mengine tofauti.

Maelezo yanayotoka na hotuba na kauli za Putin kwamba anachochewa na hisia kwamba kwa miaka mingi, nchi za Magharibi zimeidanganya Urusi, zimeidharau, na kupuuza mahitaji yake ya kiusalama.

.

Chanzo cha picha, Reuters

Maelezo ya picha, Urusi imepata hasara kubwa katika uwanja wa vita tangu Putin alipoanzisha operesheni yake maalum ya kijeshi nchini Ukraine mwaka 2022.

Je, Putin mwenyewe anaamini kwamba ametimiza wito wa Yeltsin wa "kuitunza Urusi"?

Hivi karibuni nilipata fursa ya kumuuliza swali hilo.

Baada ya mkutano na waandishi wa habari uliodumu kwa zaidi ya saa nne, Putin hatimaye alinialika kuuliza swali langu.

Nilimkumbusha rais kwamba: "Boris Yeltsin alikuambia uitunze Urusi. Lakini je, unadhani umefanya hivyo unapoangalia vifo vingi vya watu kutokana na kile kinachoitwa operesheni maalum ya kijeshi, kukaliwa kwa eneo la Kursk na vikosi vya Ukraine, vikwazo vya kimataifa, na mfumuko mkubwa wa bei? Je, unafikiri umeitunza nchi yako");