Tetesi za soka Ulaya Jumatatu: Leroy Sane njia panda Bayern

Chanzo cha picha, Getty Images
Bayern Munich hawakusudii kuboresha ofa yao ya mkataba kwa winga wa Ujerumani, Leroy Sane, licha ya mawakala wapya wa mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 29 - ambaye mkataba wake unaisha msimu huu wa joto kuwasilisha pendekezo jipya kwa mabingwa hao wa Bundesliga. (Florian Plettenberg, Sky Sports )
Mkurugenzi wa michezo wa Napoli, Giovanni Manna, anaendelea kukaa kimya kuhusu kumsajili kiungo wa Ubelgiji, Kevin de Bruyne, mwenye umri wa miaka 33, kwa uhamisho huru atakapoondoka Manchester City mwishoni mwa mkataba wake msimu huu wa joto. (Calciomercato)
Mshambuliaji wa Canada, Jonathan David, atakuwa mchezaji huru mkataba wake na Lille utakapomalizika msimu huu wa joto na mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 25 anasakwa na Napoli. (La Gazzetta dello Sport)

Chanzo cha picha, Getty Images
Bosi wa Bayer Leverkusen, Fernando Carro, anaamini kuna nafasi 50-50 kwa kiungo wa Ujerumani mwenye umri wa miaka 22, Florian Wirtz, ambaye amehusishwa na Bayern Munich, kuweza kusalia na klabu hiyo. (Sky Sports )
Beki wa kati wa Arsenal, Jakub Kiwior, yupo kwenye rada za Juventus na Inter Milan huku beki huyo wa Poland mwenye umri wa miaka 25 akipima mustakabali wake wa muda mrefu. (Football Insider), external