Misaada yamiminika kwa mwanamke aliyetamani kufa kutokana na ugumu wa maisha

fcv
Maelezo ya picha, Watu wamekuwa wakiangusha magunia ya chakula kwenye nyumba ya Shamsiyya Abubakar
  • Author, Mansur Abubakar
  • Nafasi, BBC

Shamsiyya Abubakar alikuwa ameanza kupoteza matumaini - mdororo mkubwa wa uchumi nchini Nigeria ulimfanya ahangaike kila siku kulisha familia yake ya watu tisa.

Bi Shamsiyya , mama wa mtoto mchanga, aliiambia BBC kwamba matatizo yake yamepeleka akili yake kuwa na mawazo mabaya.

"Wakati mwingine najiambia; 'badala ya kuishi hivi, si ingekuwa bora kufa");