Ukigundua una dalili hizi 10 nenda ukapimwe maradhi ya Kisukari

Chanzo cha picha, Getty Images
Afroza Akhtar hakuelewa kwamba alikuwa na kisukari kwa muda mrefu. Hakujua kwamba sababu za kujihisi kiu, uchovu na mwili kuishiwa nguvu huenda ni baadhi ya dalili za maradhi hayo.
''Nilikwenda kwa daktari na kumueleza baada ya kujisikia vibaya kwa muda mrefu.Alinifanyia vipimo vya kisukari na magonjwa mengine. Ni pale ndipo niligundulika kuwa nina ugonjwa wa kisukari kwa muda mrefu ''
Tangu hapo alianza matibabu katika hospitali maalum ya ugonjwa wa kisukari.
Si yeye pekee, kwa mujibu wa wataalamu wa kisukari, zaidi ya asilimia 50 ya watu wenye maradhi ya kisukari hawafahamu kuwa wana ugonjwa huo
Ugonjwa huo uligunduliwa wakati wa alipokuwa akipimwa maradhi mengine.
Wataalamu wanasema kutokana na hali hiyo ndiyo maana ni muhimu sana kutoa hamasa kwa jamii kuhusu ugonjwa wa kisukari.
Utafiti mmoja wa Taasisi ya Mafunzo ya Idadi ya Watu (NIPORT) unaonyesha kuwa katika jumla ya wagonjwa wa kisukari milioni 10. Miongoni mwao ni wenye umri wa miaka 18 hadi 34 ambao ni laki 2.6 na idadi ya watu zaidi ya miaka 35 ni laki 8.4.
Wataalamu wanasema kwamba ikiwa ugonjwa wa kisukari haujatambuliwa au haujatibiwa kwa muda mrefu, figo, ini na macho huharibika.
Pamoja na hayo, ngozi ya mwili huharibika, nywele hudondoka. Sehemu zingine za mwili pia zinaweza kuathirika.
"Wale wanaofanya shughuli nyingi, kama vile kutembea angalau hatua 10,000 kila siku, hata kama ana kisukari, inawezekana kudhibiti. Lakini ni wangapi wanaofanya hivyo");