'Watu hutaka kufanya ngono nami kama njia ya kunionyesha ukarimu kwa sababu mimi ni mlemavu'

Gemma Dunstan

BBC Wales Live

th

Chanzo cha picha, BBC NEWS

Maelezo ya picha, Holly anasema mahusiano mazuri kwa walemavu yanahitaji uwakilishi bora

Holly alikuwa na umri wa miaka 16 tu mtu mmoja alipomuuliza ikiwa angeweza kufanya ngono naye kwa sababu alikuwa mlemavu.

Ameulizwa maswali mengine mengi kwa miaka mingi, kama vile "anaweza kufanya ngono kwa nguvu" au ikiwa inahitajika kuwa kwenye kiti cha magurudumu akifanya ngono.

"Watu wanadhani wanakufanyia ukarimu, au hata wamejitoa mhanga kukusaidia. Jambo baya zaidi sishangai wala siudhiki tena siku hizi ninapokumbana na maswali kama hayo."

Holly, ambaye sasa ana umri wa miaka 26, ana maumivu ya muda mrefu na ugonjwa wa hypermobility na ni mmoja wa wanawake walemavu ambao wamezungumza kupinga mawazo mabaya na unyanyapaa linapokuja suala la uchumba na mahusiano.

Holly Greader alisema ni muhimu kwamba mahusiano ya furaha kwa wale ambao walikuwa walemavu yanawakilishwa.

Alianza kuchumbiana na mume wake wa sasa James alipokuwa kijana, na amekuwa naye kwa miaka tisa, na kufunga ndoa mapema mwaka huu.

"Mara nyingi katika vyombo vya habari walemavu wana maisha duni, sisi ni hadithi ya kusikitisha," alisema.

Aliongeza kuwa amekuwa akihisi kuungwa mkono naye kila wakati, lakini alihisi ubaguzi na wengine.

"Niliambiwa na watu tulipoanza kuishi pamoja mara ya kwanza, kwamba ikiwa afya yangu itadorora ataniacha.

"Kwa kuwa mzigo au kuhitaji kushughulikiwa'.

Alisema kulikuwa na mawazo ambayo watu walikuwa nayo shuleni, ambayo wengine walimuuliza hadharani.

"Inapokuja kwa watumiaji wa viti vya magurudumu, daima bila shaka ni karibu swali la kwanza, mtu huyo anaweza kufanya ngono");