Kwanini wanawake hawawezi kuwa Mapapa? na nini asili ya hili?

Chanzo cha picha, Getty Images
- Author, Muralitharan Kasi Viswanathan
- Nafasi,
- Akiripoti kutoka BBC Tamil
Wanawake hawawezi kuwa viongozi wa Kanisa Katoliki. Ukristo wa Kikatoliki haukubali wanawake kuwa makasisi. Nini msingi wa jambo hili?
Kufuatia kifo cha Papa Francis, kiongozi wa Wakristo wa Kanisa Katoliki, mchakato wa kumchagua papa mpya unakaribia kuanza. Papa mpya atachaguliwa kwa kura ya kundi la makadinali.
Lakini kulingana na Ukristo wa Kikatoliki, wanaume pekee wanaweza kuwa Papa. Kwanini, ni wanaume pekee wanaoweza kuwa makuhani kanisani?
Nafasi moja ya uongozi ambayo imeendelea bila kuingiliwa duniani kwa miaka elfu mbili iliyopita ni ile ya Papa, kiongozi wa Ukristo wa Kikatoliki.
Mtakatifu Petro, mmoja wa wanafunzi 12 wa Yesu Kristo, anachukuliwa kuwa kiongozi wa kwanza wa Ukristo wa Kikatoliki.
Jukumu hili, lililooanza naye, limeendelea bila mapumziko yoyote kwa miaka elfu mbili iliyopita.
Hadi sasa, kumekuwa na zaidi ya mapapa 250. Walakini, hakuna hata mmoja wao ambaye amekuwa mwanamke.