Tetesi za soka Ulaya Jumanne: Man City yamgeukia Reijnders

c

Chanzo cha picha, Getty Images

Manchester City inakusudia kumsajili kiungo Mholanzi Tijjani Reijnders (26) kutoka AC Milan, ambao watamuuza kama ofa ya zaidi ya pauni milioni 57 itatolewa (Telegraph)

Uongozi wa Manchester United hauna mpango wa haraka wa kumfukuza kocha wao Ruben Amorim (Talksport)

Winga wa Colombia Luis Diaz (28) ameahidi kusalia Liverpool licha ya kuhusishwa awali na Barcelona. (Express)

Real Madrid bado haijatoa ofa rasmi kwa Liverpool kumsajili beki wa kulia Trent Alexander-Arnold (26), ingawa walimuulizia wiki iliyopita kwa ajili ya Kombe la Dunia la Klabu mwezi ujao. (Sky Sports)

s

Chanzo cha picha, Getty Images

Maelezo ya picha, rent Alexander-Arnold

Liverpool inaweza kumchukua Jeremie Frimpong (24) wa Bayer Leverkusen na mholanzi, ambaye ana kipengele cha kuuzwa kwa pauni milioni 29.4-33.6. (Sky )

Skip Iliyosomwa zaidi and continue reading
Iliyosomwa zaidi