Unawezaje kufurahia tendo la ndoa katika mahusiano?

Chanzo cha picha, Getty Images
Unatathminiwa kwa mafanikio yako badala ya kile unachofanya kwa sasa. Kanuni hii pia inatumika kwa maisha ya ngono ya mtu husika.
Kuridhika kwa ngono ni hisia ya kibinafsi ambayo ni ngumu kuelezeka, na inategemea uzoefu wa mtu mwenyewe na uhusiano alionao.
Wanandoa wana mawazo tofauti kuhusu maisha yao ya ngono.
Badala ya kufafanua namna ya kufurahia ngono kwa kuzingatia ni mara ngapi unashiriki tendo la ndoa, itakuwa muhimu zaidi kuwa na uhusiano wa kihisia.

Chanzo cha picha, Getty Images
Mtaalamu wa masuala ya ngono na mwandishi wa vitabu viwili kuhusu ushiriki wa ngono vinavyouzwa sana, ambaye pia anatambuliwa katika ushauri wa masuala ya mapenzi Dk. Emily Nagoski alizungumza na BBC Mundo kuhusu suala hili.
"Mara nyingi wanandoa huenda kwa daktari kwa sababu matamanio ya kuonana kimwili na uhusiano wao haviendani," anasema Dk. Emily Nagoski.
Kulingana na yeye, baada ya kuzungumza na mamia ya wanandoa na kusikiliza maelezo ya uzoefu wao wa ngono, alishtuka kwa sababu wanandoa wengi hushiriki mapenzi kwa sababu ya kile ambacho watu wengine watasema.
Matatizo wakati wa kujamiiana
Alisema kuwa watu wengi wanaishi maisha ya unyumba bila kuchunguza kile kinachowasisimua, kinachowaridhisha, au mambo mengine yanayohusiana na kufanya mapenzi.
"Wanaelezea ngono kama wajibu wao na kuhisi kuwa tendo la ndoa hufanyika kulingana na sheria ambazo lazima zifuatwe."
Niliwafafanulia kwamba ikiwa hutaki kushiriki ngono katika uhusiano wako, sio kwamba 'una matatizo'.
"Ngono inapaswa kuwa kitu unachoweza kucheza nacho, kukufurahisha, na haupaswi kuhisi shinikizo kufanya tendo hilo."

Chanzo cha picha, Getty Images
Namna ya kuamua jinsi maisha yako ya ngono yalivyo
"Data kutoka kwa tafiti mbalimbali zinaonyesha kupungua kwa mara ambazo wanandoa wanafanya tendo la ndoa," anasema Nagoski.
"Lakini, mojawapo ya mawazo niliyoyapa kipau mbele ni kwamba kuangalia ni mara ngapi tunafanya ngono sio njia nzuri ya kuamua kama maisha yetu ya ndoa yanakwenda vizuri au la."
"Hebu fikiria, wanandoa wanaofanya mapenzi mara kwa mara, lakini mmoja wao hafurahii, ungependelea hali hiyo au wanandoa ambao hawafanyi mapenzi mara kwa mara lakini wanapofanya, wote wawili hufurahia mno");