Ndani ya ulimwengu wa "mungu wa kike" mwenye utata

Anadai kufanya miujiza, na wafuasi wake wanaamini kuwa yeye ni "mungu mwanamke."
Lakini je Radhe Ma ni nani?
Radhe Ma ni mmoja wa wanawake wachache ambao wameingia katika ulimwengu wa "miungu ya kibinadamu" nchini India, jambo lenye utata na linalokua ambalo huvutia idadi kubwa ya watu. BBC ilipata fursa adimu ya kuingia katika ulimwengu wa mwanamke huyu wanayemwona kama "mungu mwanamke", ikitafuta kufichua siri za mchanganyiko huu wa ajabu wa imani na hofu.
Wanawake waliobeba mikoba ya Louis Vuitton na Gucci, waliovaa nguo za kitamaduni za kifahari na kupambwa kwa vito vya dhahabu na almasi, hukusanyika kwa kusanyiko la jioni la Radhe Ma.
Tofauti na watu wengi watakatifu, hapendi kuamka mapema, havai nguo rahisi, hafurahii mazungumzo marefu, na anajiita "Mama wa Miujiza."
Radhe Ma aliniambia, "Miujiza hutokea kwa wafuasi wake, mahitaji yao yanatimizwa, kwa hivyo wanatoa michango."
Watu hapa wanasimulia hadithi nyingi za jinsi Radhe Ma alivyowabariki wanandoa wasio na watoto, kuwasaidia wanawake ambao walikuwa wamejifungua watoto wa kike pekee hatimaye kuzaa watoto wa kiume, kuwaponya wagonjwa, na kusaidia kuokoa biashara ambazo zilikuwa karibu kuanguka.
Madai ya nguvu za kimungu sio ya kipekee kwa Radhe Ma. India imejaa wale wanaoitwa "miungu ya kibinadamu," na ingawa hakuna takwimu sahihi rasmi, idadi yao inaonekana kuongezeka mwaka baada ya mwaka.

Baadhi yao huwakuepusha na mashtaka ya ufisadi, ukiukaji wa maadili, na hata unyanyasaji wa kijinsia. Radhe Ma alizungukwa na madai ya ushirikina (chawi) na kuwezesha malipo ya mahari, licha ya sheria ya India kukataza mazoea kama hayo. Lakini , uchunguzi wa polisi ulimalizika na mashtaka yote dhidi yake kufutwa.
Licha ya hayo, maelfu ya waja bado wanamiminika kuwaona wanaume na wanawake hawa, ambao wanachukuliwa kuwa vyombo vitakatifu, na mwaka jana, mkanyagano katika moja ya mikusanyiko hii ulisababisha vifo vya zaidi ya watu 120.
"Wahindi wengi hukulia katika familia zinazoamini kwamba nguvu za kimungu zinaweza kupatikana kupitia ibada, kutafakari, au maombi, na kwamba wale wanaozipata wana uwezo wa kufanya miujiza," anasema Shyam Manav, rais wa Shirika la India la Kupambana na Ushirikina.
Anaongeza: "Mtu kama huyo anachukuliwa kuwa kiumbe wa kimungu, au anaitwa mtakatifu
Nilikutana na Pushpinder Bhatia, mhitimu wa Shule ya Biashara ya Saïd ya Chuo Kikuu cha Oxford na mkurugenzi wa ushauri wa elimu, alipokuwa amesimama kwenye foleni ya wanawake wakisubiri kukutana na Radhe Ma. Aliniambia hakuwahi kufikiria angejikuta mwanafunzi wa "kiumbe mkuu aliyepata mwili katika umbo la mwanadamu."
Aliniambia, "Mwanzoni, nilikuwa na maswali mengi: Je, mungu anaweza kweli kupata mwili katika umbo la mwanadamu? Je, hii ni kweli? Je, kweli anaweza kutoa baraka zinazobadilisha maisha ya mtu? Na ni nini siri ya miujiza hii wanayodai kutokea");