Nchi tano, milo mitano - jinsi ya kukabiliana na gharama za chakula

Chanzo cha picha, Ben Gray
Chakula kinaendelea kuwa cha gharama ya juu, na wakati mwingine huwa haba kabisa. Kila mahali watu wanalazimika kuzoea hali mpya, na hii wakati mwingine ina maanisha kuwa wabadili kile wanachokila.
Duka la jumla la usiku la Walmart nchini Marekani
Ni alfajiri saa kumi asubuhi na tayari hali ya hewa ni ya joto kali katika msimu wa majira ya joto huko Georgia wakati Donna Martin anawasili kazini.
Siku nyingine inapoingia inamaanisha anaanza mapambano ya kuhakikisha watoto wanakula katika shule yake ya wilaya.
Bi Martin ni Mkurugenzi wa huduma ya chakula mwenye jukumu la kuwalisha wanafunzi, ambao wote wako chini ya mipango ya chakula cha bure shuleni. "Tuna maduka madogo mawili tu katika eneo yetu lenye watu 22,000," anasema. "kusema kweli ni jangwa la chakula ."
Lakini katika mwaka uliopita amekuwa akihangaika kupata kile anachokihitaji.

Chanzo cha picha, Ben Gray
Mfumuko wa bei za chakula kwa mwaka ulifika hadi 10.9% katika mwezi wa Julai, kikiwa ni kiwango cha juu zaidi cha mfumuko wa bei tangu mwaka 1979. Huku bei zikipanda baadhi ya wasamabazaji wa chakula kama vile wasambazaji wa Bi Martin hawana haja tena ya kulisha shule.
Mpango wa lishe kwa shule za shirikisho nchini Marekani unadhibitiwa vikali. Hiyo ina maanisha kuwa bidhaa kama vile chenga za mikate zinazopakwa kwenye kuku wa kukaangwa lazima zisiwe za ngano ya kukobolewa, lazima ziwe na kiwango cha chini cha sukari na chumvi. Kwahiyo Bi Martin analazimika kutafuta aina zote, kuanzia nafaka hadi chenga aina mbali mbali au yogati.
Anatambua kuwa wanaomuuzia bidhaa hizi pia wanahangaika. Ukosefu wa wafanyakazi wa muda mrefu inamaanisha kwamba hawawezi kuwapata madereva na gharama za mafuta zimeongezeka kwa 60% kwa mwaka.
- Garama ya chakula kwa mwaka nchini Marekani iliongezeka nchini kwa 10.9% mwezi Julai
- Wamarekani hutumia 7.1% ya pato lai kwa chakula(USDA 2021)
Tunda la fenesi limekua mwokozi nchini Sri Lanka

Chanzo cha picha, Chamil Rupasinghe
Kuna uhaba wa kila kitu – madawa, mafuta na chakula. Hata watu wenye kazi nzuri wanahangaika kununua bidhaa za msingi.
"Sasa watu wana wasi wasi kuhusu hali yao ya baadaye," Bi Paranathala anasema "Twanahofia hakutakuwa na chakula cha kula."
Katika Jordan, serikali ilipendekeza viwango vya bei ya kuku na bidhaa nyingine.
Wafugaji wa kuku walikubaliana na bei zilizowekwa hadi kufikia mwishoni mwa Ramadan. Lakini mwanzoni mwa mwezi Mei, walilazimika kupandisha bei, na kusababisha mfumuko wa juu.
- Mfumuko wa bei ya chakula nchini Sri Lanka kwa mwaka ulifikia 75.8% mwezi Juni
- Wasri Lanka hutumia 29.6% ya pato lao kwa chakula

Chanzo cha picha, Chamil Rupasinghe
Alianza kutengeneza supu ya binzari na nazi pamoja na matunda, badala ya mboga ambazo zingekuwa sasa ghali kununua, au nyama. Fenesi pia sasa inaonekana katika kottu – chakula maarufu cha kukaangwa kinachouzwa kama chakula cha mtaani. Na baadhi ya watu wanasaga mbegu kutengeneza mkate wa unga na keki.
Migahawa nchini inaelekea 'kutoweka'

Chanzo cha picha, Tom Saater
Kwa kawaida Emmanuel Onuorah hapendi siasa, ni muokaji, na anataka tu kuuza mikate.
Lakini hivi karibuni nchini Nigeria, kazi yake imekuwa ngumu.
"Katika mwaka uliopita, unga wa ngano umepanda kwa zaidi ya 200%, sukari imepanda kwa karibu 150%, mayai ambayo tunatumia yamepanda kwa takriban 120%," anasema.
"Tunaendesha biashara kwa hasara," anasema. Amelazimika kuwafuta kazi wafanyakazi wake 305 kati ya 350. "Watalisha vipi familia zao");