Hatima ya tamasha la 'kwanza na kubwa zaidi' la ngono nchini Korea
Na Jean Mackenzie ,
Mwandishi wa Seoul

Chanzo cha picha, Play Joker
Lee Hee Tae alikuwa na matumaini makubwa kwa tamasha lake la ngono, ambalo aliliita kwa fahari kama "La kwanza na kubwa zaidi" nchini Korea Kusini.
Alitarajia mashabiki 5,000 wangemiminika kuona waigizaji wa filamu za ponografia wa Kijapani wanaowapenda, ambao walikuwa wakisafirishwa kwa ndege kwa ajili ya tukio la wikendi iliyopita. Kulikuwa na maonyesho ya mitindo .
Lakini zikiwa zimesalia saa 24 tu, tamasha hilo lilifutiliwa mbali.
Korea Kusini inajulikana kwa mtazamo wake wa kihafidhina wa ngono na burudani ya watu wazima. Utupu wa hadharani na maonyesho ya aina hiyo yamepigwa marufuku, na ni kinyume cha sheria kuuza au kusambaza filamu za watu wazima ingawa sio marufuku kuzitumia.
"Takriban kila nchi iliyoendelea huwa na tamasha la ngono, lakini hapa Korea Kusini hatuna hata utamaduni wa burudani ya watu wazima. Nataka kuchukua hatua za kwanza za kuunda moja," alisema Lee Hee Tae, ambaye kampuni yake ya Play Joker iliunda filamu kama hizo zisizo na makali -kabla ya kuanza kupanga hafla na shughuli zinazohusiana na aina hiyo ya burudani .
Mwezi mmoja kabla, vikundi vya kutetea haki za wanawake kutoka mji wa Suwon, ambako tukio hilo lilipaswa kufanyika, walijitokeza kupinga. Walishutumu tamasha hilo kwa kuwatumia vibaya wanawake katika nchi ambayo unyanyasaji wa kijinsia umeenea.
Walibishana kwamba hii haikuwa tamasha iliyolenga jinsia zote mbili. Maonesho ya wanawake waliovalia mavazi duni ulipendekeza walio na tikiti wanaweza kuwa wanaume kwa wingi.
Meya wa eneo hilo alilaani tukio hilo kwa kufanyika karibu na shule ya msingi na mamlaka ilitishia kunyang'anya leseni ya ukumbi huo ikiwa itaendelea. Ukumbi baadaye ulikataa kuwa mwenyeji .
Akiwa amechanganyikiwa, lakini bila kufadhaika, Bw Lee alibadilisha maeneo, lakini msururu wa matukio sawa ulijitokeza. Mamlaka hiyo mpya ilishutumu tamasha hilo kwa "kuweka mtazamo potovu wa ngono" na kusisitiza kuwa ukumbi huo ughairi. Kisha, Bw Lee alipata meli iliyotiwa nanga kwenye mto huko Seoul. Lakini, kufuatia shinikizo kutoka kwa baraza hilo, mkodishaji wa boti hiyo alitishia kuizuia na kukata umeme ikiwa promota wake ataruhusu tamasha hilo kuendelea.
Katika kila upande, Bw Lee alilazimika kupunguza tamasha huku wenye tikiti wakiitisha kurejeshewa hela zao, na kumgharimu mamia ya maelfu ya pauni.

Chanzo cha picha, Play Joker
Akiwa hana chaguo jingine, alipata baa ndogo ya chini ya ardhi katika kitongoji cha Gangnam huko Seoul, ambayo inaweza kubeba karibu watu 400. Wakati huu aliweka eneo hilo siri.
Kwa hivyo, baraza la Gangnam liliandikia kila moja ya mamia ya mikahawa yake likiwaonya kuwa litafungwa ikiwa wataandaa tamasha hilo, likishutumu kuwa "linaeneza madhara kwa maadili". Lakini baa ilisimama kidete.
Kisha, siku moja kabla, nyota wa filamu za watu wazima kutoka Japan waliojiondoa. Shirika lao lilisema msukosuko kwenye tamasha "umefikia kiwango cha juu" na wanawake walikuwa na wasiwasi wanaweza kushambuliwa na hata kuchomwa visu.
Kutoka ofisini kwake Gangnam, Bw Lee aliambia BBC kwamba alishtushwa na matukio ambayo yalikuwa yamefanyika kwa "njia isiyoweza kufikirika", akiongeza kwamba alipokea vitisho vya kuuawa. "Nimechukuliwa kama mhalifu bila kufanya chochote kinyume cha sheria", alisema, na kusema kuwa tamasha hilo halikuvunja sheria .
Play Joker iliandaa hafla zenye kuvutia hapo awali. Mwaka jana walifanya gwaride la wanawake katika mitaa ya Seoul aakiwa amevalia karatasi za kadibodi, akiwaalika wapita njia kuweka mikono yao ndani na kugusa matiti yake.
Bw Lee anasema anataka kupinga mitazamo ya Korea kuhusu ngono na ponografia, ambayo imesalia kuwa ya zama za kale.
"Mamlaka ni wanafiki. Ukiingia mtandaoni kila mtu anashiriki ponografia, basi watu wanatoka na kujifanya hawana hatia. Je, tutaendelea na udanganyifu huu hadi lini");