Jinsi ya kugundua ulaghai wa ofa za kazi kwenye WhatsApp na nini cha kufanya ili kuziepuka

g

Chanzo cha picha, Getty Images

Na Dario Brooks

BBC News World

Ujumbe wenye nambari kutoka nchi isiyojulikana na unaotoa mapato kwa kazi rahisi, pia ulifika kwenye WhatsApp ya David Guzmán.

Kama ilinavyotokea kwa maelfu ya watu duniani, aina hizi za ujumbe zilibadilika kwa kiasi fulani: "Mara kadhaa nilipokea ujumbe kutoka nambari nisiyoijua, kutoka Uchina au ," Guzmán anaiambia BBC.

"Siku moja nilisema, 'Sawa, nini kinaweza kutokea'. Ujumbe unasema kwamba wanakualika kufanya kazi kwenye jukwaa katika mji wa Wuhan, Uchina, na wanataja mtandao wa kijamii, sawa na TikTok ," anaelezea miaka 24.

Kazi ilijumuisha sharti la "kupenda" video na kutuma picha ya skrini kama uthibitisho. Kwa kufanya hilo ungepata malipo kwa akaunti yako ya benki.

"Kisha nikasema 'Ni sawa kuweka likes chache , sawa? Ni nini kibaya zaidi kinachoweza kutokea");