Mkutano wa siri uliojaribu kuzuia vurugu za muziki wa kufoka

df

Chanzo cha picha, Getty Images

Maelezo ya picha, Tupac Shakur aliuawa kwa kupigwa risasi mwaka 1996 akiwa na umri wa miaka 25
  • Author, Ian Youngs
  • Nafasi, BBC News World

Kabla ya mvutano wa waimbaji wa kufoka foka (rapa) kutoka mashariki na magharibi katika miaka ya 1990 kuchemka na mauaji ya Tupac Shakur na Notorious BIG, mtayarishaji mashuhuri wa muziki Quincy Jones aliitisha mkutano wa siri ambapo alitoa wito wa kukomesha vurugu hizo.

Muziki wa hip-hop (kufoka foka) ulizidi kupata umaarufu kutoka mtaani hadi kwenye majukwaa makubwa katika miaka ya 90.

Quincy Jones alikuwa katika magenge na alidungwa kisu akiwa na umri wa miaka saba katika miaka ya 1930 huko Chicago, kabla ya kuwa gwiji wa muziki wa Marekani kutokana na kufanya kazi na magwiji kama Ray Charles, Frank Sinatra na Michael Jackson.

Alikuwa kiini cha mapinduzi katika muziki wa jazz, swing, soul, funk, disco na pop - lakini eneo moja la maisha yake ambalo halijazingatiwa sana hadi alipofariki wiki iliyopita akiwa na umri wa miaka 91 - ni nafasi yake katika hip-hop.

Pia unaweza kusoma

Jones aliheshimiwa katika pembe zote za muziki, ikiwa ni pamoja na muziki wa kufoka foka ama hip-hop.

Alifanya kazi na wasanii maarufu wa rapa katika miaka ya 80, na katika miaka ya 90 aliitambua hatari iliyoibuka katika ushindani tete kati ya lebo na nyota wa muziki huo.

Kwa hivyo aliwaleta wasanii, watendaji wakuu na wazee wa jamii ya Wamarekani weusi pamoja kwa mkutano wa siri mwaka 1995, akitumai itakuwa hatua ya mabadiliko.

Ushindani wa Muziki

K

Chanzo cha picha, Getty Images

Maelezo ya picha, Notorious BIG alisajiliwa na P Diddy, kwenye lebo ya Bad Boy

Pwani ya mashariki ilikuwa ni nyumbani kwa muziki wa hip-hop. Mwaka 1992, Sean Combs - wakati huo akijulikana kama Puffy na baadaye kama P Diddy - alizindua lebo yake ya muziki ya Bad Boy huko New York na wasanii akiwemo Notorious BIG, aka Biggie Smalls.

Wakati huo huo, Los Angeles ilikuwa ikichupikia kama jiji la muzuki wa kufoka, likiongozwa na lebo tishio ya Suge Knight, Death Row Records, ambayo pia ilikuwa na wasanii Dr Dre na Tupac.

Mwaka 1994, Tupac alipigwa risasi na kujeruhiwa wakati wa uporaji kwenye ukumbi wa studio. Baadaye alidokeza kwamba rafiki yake wa zamani Biggie huenda alifahamu kuhusu shambulio hilo mapema. Kisha Biggie akatoa wimbo wa Who Shot Ya? Ambao Tupac alifikiri kuwa unamhusu.

Mkutano wa siri

SDXC

Chanzo cha picha, Madison McGaw/BFA.com/Shutterstock

Maelezo ya picha, Quincy Jones alimwomba Fab 5 Freddy kuwa msimamizi katika mkutano wa 1995

Jones, wakati huo akiwa mmiliki wa jarida, Vibe, aliitisha mkutano 1995. Ugomvi wa mashariki-magharibi haikuwa sababu pekee ya Jones kuitisha mkutano - alikusudia pia kujadili hali ya hip-hop na kuruhusu kizazi kipya kusikia ushauri wa maisha na biashara kutoka kwa kundi la watu weusi waliofanikiwa.

Lakini taswira mbaya ya hip-hop na mivutano iliyokuwa ikiongezeka - lilikuwa jambo kubwa la kuzungumzwa.

Jones aliuambia mkutano huo: "Kitu ambacho kinaniumiza sana – ni kuhusu Tupac."

Tupac hakuwepo wakati huo - alikuwa gerezani kwa unyanyasaji wa kingono. Suge na Dre walikuwepo, pia Combs na Biggie.

Jones tayari alikuwa amepitia ugomvi wake mwenyewe na Tupac – rapa huyo alimkosoa mtayarishaji huyo katika toleo la 1993 la jarida la Source kwa kuoa wanawake weupe.

"Hatimaye tulipatana, ingawa hali ilikuwa ya mvutano hapo mwanzo," Jones alisema kwenye hafla hiyo.

"Mwishowe tulizungumza, na akasema hakuna mtu aliyezungumza naye kama hivyo hapo awali. Na nikasema, siwezi kuvumilia. Kwa sababu hatuwezi kushindwa kuzungumza."

ER

Chanzo cha picha, Amamy

Maelezo ya picha, Toleo la 1994 la jarida la Vibe lilikuwa na kichwa cha habari "Je, Tupac ni kichaa au haeleweki tu");