Je, Kanisa Katoliki linaingilia siasa za Tanzania?

S

Chanzo cha picha, TEC

  • Author, Sammy Awami
  • Nafasi,
  • Akiripoti kutoka BBC Dar es Salaam

Kanisa Katoliki nchini Tanzania ni miongoni mwa taasisi zilizo mstari wa mbele katika kuzungumzia masuala ya kiraia, kisiasa na kijamii.

Wakati nyakati zingine jukumu hili hufanywa kupitia mwamvuli rasmi wa Baraza la Maaskofu TEC, nyakati zingine hufanywa na askofu mmoja mmoja kwa nafasi zao za uongozi wa kanisa.

Bila shaka ni sehemu ya sababu kwanini tukio la kushambuliwa kwa Katibu Mkuu wa Baraza la Maaskofu wa Kanisa Katoliki Tanzania (TEC), Padri Charles Kitima limeibua huzuni na ukosoaji na pia kuhusianishwa na ukosoaji unaofanywa na Kitima na TEC.

"Kitima alikuwa anakosoa wakati wa Magufuli. Hajawahi kukaa kimya akiona UOVU. Wakati wa Magufuli hakuna aliyemgusa. Swali: Mnadhani sasa mapadri watakaa kimya maana mshawatia uwoga? Tanzania ina amka na huzuni leo" ameandika mwanasheria na Mtetezi wa Haki za Binadamu Fatma Karume katika ukurasa wake wa X.

"…kwa kweli walilenga kumdhulumu maisha yake, kwa sababu wamempiga sehemu za kichwa, na walimpiga zaidi ya mara moja kwa nia ya kutaka kumuua au kumjeruhi vibaya… ni shambulio lililofanywa na mtu mwenye ujuzi wa alichokuwa anakifanya… halikuwa shambulio la kihalifu la kawaida," Rais wa Chama cha Wanasheria Tanganyika, Boniface Mwabukusi ameieleza BBC baada ya kumtembelea Padri Kitima hospitalini.

Tazama hapa