Jinsi Wahindi wawili walivyotoweka usiku wa Julai nchini Kenya

Khan

Watalii wawili wa Kihindi na dereva wao wa ndani walitoweka katika mji mkuu wa Kenya, Nairobi, usiku wa Julai.

Zaidi ya miezi miwili baada ya tukio hilo, polisi tisa wamekamatwa kuhusiana na kesi hiyo, ambayo India inasema "inaifuatilia kwa karibu".

BBC imeweka pamoja matukio yaliyojiri kuelekea kutoweka kwao na kujaribu kufumba fumbo hilo kwa kuangazia maswali mengi ambayo hayajajibiwa.

Katika moja ya machapisho yake ya mwisho kwenye mitandao ya kijamii kabla ya kutoweka, Zulfiqar Ahmad Khan alishirikisha video ya simba anayenguruma katika mbuga ya wanyama ya Maasai Mara nchini Kenya ambako alikuwa akipumzika.

"Asubuhi ya kichawi huko Maasai Mara. Hebu fikiria mara ya kwanza kukutana na Simba. Kiamsha kinywa cha mtu yeyote");