Waridi wa BBC : Nilikimbia ‘dogoli na okuleya’ kutimiza ndoto yangu ya kuwa sauti ya jamii

Mkurugenzi TWAWEZA

Chanzo cha picha, Annastazia Rugaba

Maelezo ya picha, Mkurugenzi wa Idara ya Utetezi -TWAWEZA Afrika Mashariki
  • Author, Esther Namuhisa
  • Nafasi, BBC Swahili
  • Twitter,
  • Akiripoti kutoka Dar es Salaam
  • Kipande cha gazeti kilichofungia sabuni kilivyonipa taarifa ya thamani
  • Bosi wangu alivyochana barua na kuifuta ajira yangu

Kutoka katika kisiwa cha Ukerewe kinachopatikana katika ziwa Victoria kaskazini magharibi mwa Tanzania ndipo alikozaliwa na kukulia Annastazia Rugaba, 40 ambaye simulizi ya safari ya kuifikia ndoto yake kuwa sauti ya jamii imejaa vizingiti vingi alivyokabiliana navyo akiwa mtoto wa kike.

Annastazia ambaye kwa sasa ni Mkurugenzi wa Idara ya utetezi katika taasisi ya kiraia ya Afrika mashariki TWAWEZA, amezungumza na Esther Namuhisa namna mila potofu, unyanyasaji wa kijinsia na fikra hasi vilivyompa ari ya kupigania hatma yake kupitia elimu.

m

Chanzo cha picha, Anna Rugaba

Alizaliwa katika mazingira ya mapambano. Mara tu baada ya baba yake kufariki na mama yake kubaki mjane aliyepoteza urithi kwa wakwe zake bila usaidizi wa malezi kwa watoto.

Akiwa mtoto wa tano, aliyekosa malezi ya baba tangu akiwa na umri wa miaka mitatu, hakutarajiwa kuwa angefika katika hatua aliyofikia sasa.

“Kwa sasa naweza kusema nimejipata lakini natamani vijana waanze kujitafuta mapema na si wakiwa na miaka 40 kama mimi”

Skip Iliyosomwa zaidi and continue reading
Iliyosomwa zaidi