‘Hatuonekani katika nchi yetu wenyewe': Kuwa Muislamu katika India ya Modi

Chanzo cha picha, GETTY IMAGES
- Author, Soutik Biswas
- Nafasi, BBC
Miaka sita iliyopita, mvulana Mwislamu alirudi akiwa na uso mwekundu kutoka shule maarufu katika mji wa kaskazini mwa India wa Agra.
"Wanafunzi wenzangu waliniita gaidi wa Pakistan," mtoto wa miaka tisa alimwambia mama yake.
Reema Ahmad, mwandishi na mshauri nasaha, anakumbuka siku hiyo vizuri.
Wakati akiwa darasani baada ya mwalimu kutoka nje. Kundi la moja la wavulana lilimnyooshea kidole na kusema, 'Huyu ni gaidi wa Pakistani. Muueni!
Alifichua kuwa baadhi ya wanafunzi wenzake walimwita mdudu. Bi Ahmad hatimaye alimtoa mwanawe shuleni hapo. Kwa sasa mtoto huyo wa miaka 16 anasoma nyumbani.
"Nilihisi mshituko kupitia uzoefu wa mwanangu, hisia ambayo sikumbuki kuwa nayo katika ujana wangu nikikulia hapa," anasema.
"Kuwepo darasani kulitulinda kama Waislamu. Lakini sasa, inaonekana darasa na fursa inayokufanya kuwa shabaha iliyo wazi zaidi."
Kuna Chuki dhidi ya Waislamu?

Chanzo cha picha, Bimal Thankachan
Tangu Waziri Mkuu, Narendra Modi ambaye ni mzalendo wa Kihindu wa chama cha Bharatiya Janata Party (BJP) alipoingia madarakani mwaka 2014, Waislamu milioni 200 wa India wamekuwa na safari yenye msukosuko.
Makundi ya Wahindu yamewaua washukiwa wa biashara wa ng'ombe na kulenga biashara ndogo ndogo zinazomilikiwa na Waislamu.
Maombi yamewasilishwa dhidi ya misikiti. Mashambulizi ya mtandaoni dhidi ya wanawake wa Kiislamu. Vikundi vya mrengo wa kulia na baadhi ya vyombo vya habari vya vimechochea chuki dhidi ya Uislamu kwa shutuma za jihad.
Kwa mfano, kuwashutumu kwa uwongo wanaume wa Kiislamu kuwabadilisha dini wanawake wa Kihindu kwa ajili ya ndoa.
Na matamshi ya chuki dhidi ya Waislamu yameongezeka - robo tatu ya matukio yaliripotiwa kutoka majimbo yanayotawaliwa na chama cha BJP.
"Waislamu wamekuwa raia wa daraja la pili, na hawaonekani katika nchi yao," anasema Ziya Us Salam, mwandishi wa kitabu kipya, Being Muslim in Hindu India.
Bi Ahmad - ambaye familia yake imeishi katika eneo la Agra kwa miongo kadhaa, akiwa na marafiki wengi wa Kihindu katikati mji huu uliojaa nyumba - anahisi kuna mabadiliko.
Mwaka 2019, Bi Ahmad alijitoa katika kikundi cha WhatsApp cha shule ambapo alikuwa mmoja wa Waislamu wawili tu. Hii ilifuatia kutumwa kwa ujumbe baada ya India kuanzisha mashambulizi ya anga dhidi ya wanamgambo huko Pakistan yenye Waislamu wengi.
"Ikiwa watatupiga kwa makombora, tutaingia kwenye nyumba zao na kuwaua," ujumbe kwenye kundi hilo ulisema, ukirejelea maneno ambayo Modi alisema kuhusu kuua magaidi na maadui wa India ndani ya nyumba zao.
Nilipoteza uvumilivu. Niliwaambia marafiki zangu mna matatizo gani? Je, mnaunga mkono mauaji ya raia na watoto");