Jinsi kujiuzulu kwa kamanda wa RSF kulivyopelekea mauaji ya kimbari Sudan

Aliyekuwa kamanda wa kikosi cha kukabiliana na dharura Abu Keikal alivyoasi uaminifu wake na kutoka katika jeshi la Sudan

Chanzo cha picha, Social media

Maelezo ya picha, Aliyekuwa kamanda wa kikosi cha kukabiliana na dharura Abu Keikal alivyoasi uaminifu wake na kutoka katika jeshi la Sudan

Uchambuzi wa BBC ulivyoangazia video za wapiganaji wakijivunia mauaji na kisha wakicheka waathiriwa, imebaini kwamba waliotekeleza mauaji hayo ni wanachama wa Kikosi cha kukabiliana na dharura (RSF) cha Sudan.

BBC imethibitisha kwamba watu 80 waliuawa kwenye shambulio la Oktoba katika mji wa al-Seriha, jimboni Gezira, huku Umoja wa Mataifa ukiripoti idadi ya vifo inaweza kufikia 124.

Mauaji haya yalitokana na kutoroka kwa kamanda mkuu wa RSF.

Mauaji haya yanadhihirika kuwa ni kulipiza kisasi baada ya kamanda mkuu wa RSF, Abu Keikal, kutoroka na kujiunga na jeshi la Sudan.

Hii ilitokea mnamo Oktoba 20, na kusababisha mashambulizi ya kulipiza kisasi katika vijiji vya Gezira hadi mwezi Novemba 4.

Skip Iliyosomwa zaidi and continue reading
Iliyosomwa zaidi