Kuimarisha ulinzi mitaani si suala baya- Polisi Tanzania yasema

Maelezo ya video, Sidhani kuimarisha ulinzi mitaani ni suala baya- Kamanda Muliro
Kuimarisha ulinzi mitaani si suala baya- Polisi Tanzania yasema

Kamanda wa Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam, Jummane Muliro amepuuzilia mbali madai kwambo polisi wamezingira nyumba za viongozi wa chama kikuu cha Upinzani nchini Tanzania Chadema.

Akizungumza na mwandishi wa BBC Regina Mziwanda Bw. Muliro alisema polisi wameimarisha usalama katika mitaa ya Dar es Salaam kabla ya Pasaka na haelewi kwanini baadhi ya watu wanajitia hofu kufuatia hatua hiyo. Msikilize.