Mwanamke mwenye Watoto 19 asimulia changamoto zinazomkabili

Maelezo ya video, Mwanamke mwenye Watoto 19 asimulia changamoto zinazomkabili

Mwanamke mmoja mwenye umri wa miaka 49 kutoka eneo la Kilifi, pwani ya Kenya amejaliwa watoto 19.

Mboze Munga Chiro ana watoto 10 wa kiume na 9 wa kike. Mtoto wake wa kwanza ana miaka 32 na kitinda mimba ana miaka miwili.

Amekuwa akijaliwa mtoto kila mwaka na kwa bahati nzuri watoto wake wana afya nzuri, ingawa alimpoteza mtoto mmoja wa kike.