Waridi wa BBC: Ummy Dolly, mlimbwende ambaye chakula chake ni mende

- Author, Anne Ngugi
- Nafasi, BBC Swahili
Baadhi ya wadudu hutajwa kuwa chakula bora chenye protini na kilicho chenye ladha nzuri katika jamii mbalimbali.
Takriban spishi 20,000 za wadudu huliwa na mataifa kama ya Asia, Amerika Kusini na hata sehemu zingine za Afrika.
Nchini Tanzania, kuna jamii ambazo kula wadudu kama senene, panzi na kumbikumbi ni jambo la kawaida, lakini ukiuliza juu ya mende kuwa chakula ni jambo la kustaajabisha.
Saumu Hamisi ambaye anajulikana kama Ummy Doll , ni msichana mwenye miaka 20 kutoka nchini Tanzania, anayeishi eneo la pembezoni mwa bahari Kigamboni Daresalam .