Burundi: Jinsi Charlotte na Gabin walivyooana hospitalini

Charlotte na Gabin

Ukiulizwa uelezee ni mambo gani ambayo hufanyika hospitalini, bila shaka harusi haitakua miongoni mwa mambo utakayoyataja, ila mambo yalikua tofauti kwa wapenzi hawa wa Burundi.

Charlotte Mukantwari na Gabin Ndayizigiye ni wakazi wa wilaya ya Kirundo Kaskazini mwa Burundi, kwao hakuna jambo ambalo lingewazuia kufunga pingu za maisha hata kama ni hospitalini.

Baada ya bwana harusi mtarajiwa Gabin kupata ajali mwanzoni mwa wiki iliyopita ambapo walikua wamepanga harusi yao ifanyike, alijiuliza mengi.

"Baada ya kupata ajali… niliwaza kwamba: 'Ni shetani ambaye hataki nioe");